Breaking News

News Hofu ya virusi vya Zika yamfanya Rihanna aahirishe kutumbuiza Colombia

wp-1467572465132
Tamasha la Lollapalooza Colombia limeahirishwa baada ya Rihanna aliyekuwa atumbuize kama msanii mkuu, kujiondoa na kuwafanya waandaji wakose muda wa kutafuta msanii mbadala.Pamoja na kwamba Lollapalooza wameshindwa kumtaja Rihanna, vyombo vya habari vimeripoti kuwa aliahirisha kutokana na hofu ya virusi vya Zika.
Rihanna 2013

Tamasha la Lollapalooza lilianzia kufanyika Chicago peke yake kabla ya kupanuka hadi Chile mwaka 2011. Tangu hapo limekuwa likifanyika Brazil, Argentina, na Germany.
Mwaka huu ilikuwa ni mara ya kwanza kuanza kufanyika Colombia.
Wasanii wengine ambao wangetumbuiza ni Lana del Rey, Disclosure, Wiz Khalifa na wengine. Lilikuwa limepangwa kufanyika Sept. 17 na 18 mjini Bogotá.
Kwa sasa wanarudisha fedha kwa watu walionunua tiketi.

No comments