Breaking News

News Rais Magufuli kateua wakuu wa wilaya 139, mabadiliko madogo kwa wakuu wa mikoa



Taarifa kutoka Ikulu ya Tanzania leo June 26 inasema Rais John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko kwenye nafasi za wakuu wa Mikoa pamoja na wakuu wa Wilaya,kwenye mabadiiko hayo amewateua jumla ya wakuu wa wilaya 139.
Mabadiliko haya yanamhusu aliyekua mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi.Zainab R. Telack kuwa mkuu mkoa wa Shinyanga  ambaye anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekua mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi.Anna Kilango Malecela.
Mwingine aliyehusishwa na mabadiliko haya ni pamoja na Dkt Binilith Satano Mahenge kuwa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Satano anajaza nafasi ilyoachwa wazi na aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambapo atapangiwa majukumu mengine.
Mwingine  aliyeteuliwa ni Dkt. Charles F Mlingwa ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Mara  na anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw.Stanslaus Magesa Mulongo  ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Nimeipata pia List ya wakuu wa Wilaya wapya mtu wangu nimekuwekea na List ya wilaya zao.
1
2
3
4
5
6
7
8
Kilichomchekesha Rais Magufuli japokuwa alikua kavaa sura ya kazi IKULU

No comments