Pedro Pablo Kuczynski bado anaongoza uchaguzi Peru
Huku karibu asilimia 90 ya kura zikiwa zimehesabiwa kwenye uchaguzi wa urais nchini Peru, afisa mkuu wa zamani wa Benki ya Dunia Pedro Pablo Kuczynski, anaongoza kw kura chache dhidi ya mpinzani wake Keiko Fujimori.
Bwana Kuczynski anaongoza kwa asilimia moja mbele ya Bi Fujimori na kusababisha mshindi kutotangazwa mapema.
Waandishi wa habari wanasema kuwa sakata za hivi majuzi za ufisadi, zimeathiri umaarufu wa Bi Fujimori, ambaye ni bintiye rais wa zamani aliye gerezani Alberto Fujimori.
No comments