Aliyepanga kushambulia mechi akamatwa Ukrain
Wapelelezi nchini Ukraine wanamzuilia raia mmoja wa Ufaransa, anayesemekana alikuwa akipanga misururu ya mashambulio, katika mashindano ya soka barani Ulaya ya mwaka huu wa 2016, yatakayofanyika katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris.
Idara hiyo ya ujasusi inasema kwamba mwanamume huyo alinaswa mwezi Mei katika mpaka kati ya Ukraine na Poland.
Inasemekana kuwa alikamatwa akiwa na kasha kubwa lililojaa silaha mbalimbali, zikiwemo bunduki ya rashasha na magruneti yanayorushwa kwa kutumia bunduki.
Mashindano hayo ya Euro 2016, yanangoa nanga siku ya Ijumaa.
No comments