Breaking News

Wanasayansi kukuza viungo vya binadamu ndani ya nguruwe



Wanasayansi nchini Marekani wanajaribu kukuza viungo vya binadamu ndani ya mwili wa nguruwe, wakitumia teknolojia mpya inayofahamika kama 'Gene Editing'.
Wanasayansi hao wametoa vinasaba vinavyosaidia ukuaji wa kongosho kwenye nguruwe na badala yake wanaweka chembe chembe za viungo vya binadamu kwa matarajio kuwa kongosho ya binadamu itakua.
Wataalamu katika chuo kikuu cha California, Davis wanaamini kuwa utafiti huo utasaidia kupunguza uhaba wa viungo vya binadamu.
Hata hivyo teknolojia hiyo mpya inapingwa vikali na wanasayansi wengine kwa sababu ya maadili ya udaktari.
Wanasayansi hao wanadai kuwa huenda chembe chembe za binadamu zitakuwa na kufika kwenye ubongo wa nguruwe unaoendelea kukuwa.

No comments