Breaking News

VIDEO: TRA yafafanua 18% ya VAT kwenye huduma za kifedha



Leo July 01 2016 Mamlaka ya mapato Tanzania ‘TRA imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa za upotoshaji kuhusu marekebisho ya sheria ya kodi ya ongezeko la thamani ‘VAT’ ya mwaka 2014. Kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania ‘TRA’, Alphayo Kidata amezungumza na waandishi wa habari na kusema….
>>>’kuna taarifa ambazo si za kweli zinazoenezwa kupitia mitandao ya kijamii kuwa VAT itatozwa kwanye amana ya mwenye fedha kwenye benki. Hii siyo kweli, ukweli ni kuwa kiasi cha VAT kitakachotozwa ni asilimia 18 ya kiasi  cha gharama ya huduma iliyotolewa na benki au taasisi yoyote ya fedha’.

No comments